alt text

B-Carotene & Lycopene Capsule


Viungo:

B-Carotene, Lycopene

B-Carotene & Lycopene Capsule

Kazi Na Faida Zake



Yafaa Kutumiwa Na:


Maelezo Muhimu:

Ufanyaji Kazi Wa B-Carotene Kama Vitamini A
B-carotene ni rangi ya asili (nyekundu-rangi ya chungwa) ndani ya karoti inayozifanya kuwa na rangi ya chungwa na ndiyo namna carotene inavyokuwa katika mimea. Molekuli moja ya B-carotene huweza kuvunjwa na vimeng'enya vilivyoko ndani ya utumbo na kupata molekuli mbili za vitamini A, ambayo huchochea kujigawa kwa seli, husaidia mwili kukua, na huongeza kasi ya kujikarabati kwa seli za tishu zinazofunika viungo vya ndani ya mwili (epithelial tissue) na ukuaji wa sebum. Ni muhimu kwa ukuaji wa mifupa, meno, watoto na kulinda uwezo wa kuona.

Tabia Za B-Carotene & Lycopene Kama Antioxidant
Kwa kuwa ni mchanganyiko muhimu wa flavonoid, B-Carotene ina tabia za nguvu za antioxidant, inasaidia kupambana na radikali huru na hivyo kupunguza madhara yake kwenye utando unaofunika seli, DNA na protini kwenye seli. Lycopene ni carotene ng'avu nyekundu inayopatikana ndani ya nyanya na ndani ya matunda na mboga nyingine nyekundu. Umbo la lycopene linairuhusu kushambulia radikali huru kirahisi kutoka maeneo yanayoizunguka, na kuifanya kuwa antioxidant ya nguvu.

Tabia Za Kuzuia Kansa Za B-Carotene & Lycopene
B-Carotene huzuia carcinogen zisishambulie DNA kwenye kiini cha seli. Huzuia kusambaa kwa seli za kansa hivyo kuzuia kansa kuhama kutoka sehemu moja hadi nyingine. Ripoti ya kisayansi iliyoandaliwa na mabingwa wa tiba wa Marekani mwaka 1989 inaonyesha kuwa lycopene huzuia ukuaji wa saratani ya tezi dume.

Kuifanya Damu Kuwa Nyepesi
Lipids zilizomo ndani ya damu mara nyingi ni triglyceride, cholesterol, phospholipids. Nyingi ya hizi huungana na protini na kujenga lipoprotein ambayo huganywa katika makundi mawili, low density lipoprotein (LDL) na high density lipoprotein (HDL).
Ikiwa kiwango cha LDL katika damu kitakuwa kikubwa, kipenyo cha arteri kitakuwa kidogo, atherosclerosis hutokea na uwezekano wa kupata mshituko wa moyo (heart attack) huwa mkubwa. Hii ndiyo sababu LDL huitwa "bad cholesterol".
Kiwango kikubwa cha HDL hulinda dhidi ya magonjwa ya moyo kwa kutoa LDL nje ya mfumo wa damu. Hii ndiyo sababu HDL huitwa "good cholesterol". B-Carotene na lycopene vyote huwasaidia watu wenye umri mkubwa kuzuia kuganda kwa damu na kupunguza uwezekano wa kupata mshituko wa moyo.

B-Carotene & Lycopene





<<<<< MWANZO